CHAMA CHA WAHITIMU WAJASIRIAMALI TANZANIA
Graduate Entrepreneurs Association – GEA
Tunaunganisha Wahitimu Wajasiriamali Tanzania.
Jukwaa la pamoja la wahitimu wa vyuo vikuu na vyuo vya kati walioamua kujiajiri, kujenga biashara, kushirikiana na kutengeneza fursa.
Kuhusu
Kuhusu GEA
GEA Tanzania — Kuunganisha Wahitimu Wajasiriamali Tanzania Nzima. GEA ni jukwaa linalowaunganisha wahitimu wa vyuo vikuu na vyuo vya kati walioamua kujiajiri kupitia ujasiriamali: kubadilishana uzoefu, kupata fursa za biashara, mitaji, masoko, mafunzo, urasimishaji, na sauti ya pamoja. GEA inaanzia Iringa kama eneo la majaribio, kabla ya kupanuka katika mikoa yote ya Tanzania.
Faida
Kwa nini ujiunge
Faida za uanachama wa kitaifa — mitandao, rasilimali, na sauti ya pamoja.
Networking
Ungana na wahitimu wajasiriamali kote nchini.
Mitaji
Pata mwongozo na uhusiano wa fursa za mtaji.
Ukuaji
Kua biashara yako kupitia ushauri na ushirikiano.
Masoko
Panua soko kupitia mtandao wa kitaifa wa GEA.
Mafunzo
Mafunzo ya biashara, uongozi, na ujuzi wa kisasa.
Sauti
Uwakilishi wa pamoja wa maslahi ya wajasiriamali wahitimu.
Dira
Kuwa chama kinachoongoza cha wajasiriamali wahitimu kinachochochea ukuaji wa kiuchumi na kijamii nchini Tanzania.
Dhamira
Kuwawezesha wanachama kupitia mafunzo, mitandao, uongozi, na fursa za biashara kwa ajili ya maendeleo endelevu.
Malengo
1. Kuunganisha wajasiriamali wahitimu kote nchini. 2. Kutoa mafunzo na ushauri wa biashara. 3. Kuendeleza uongozi na uwakilishi wa wanachama. 4. Kuwezesha ushirikiano na uwekezaji.
Uanachama
Jinsi ya kujiunga
-
01
Jaza fomu ya maombi mtandaoni
-
02
Wasilisha taarifa na ridhaa ya PDPA
-
03
Subiri ukaguzi wa ofisi ya GEA
-
04
Pokea namba na kadi ya kidijitali
Mtandao wa Kitaifa
GEA ni chama cha kitaifa
Tunajenga miundombinu ya uanachama kwa mikoa yote ya Tanzania. Pilot ya awamu ya kwanza inaanzia Iringa, kisha kupanuka kitaifa.
- Wanachama
- 1
- Mikoa (active)
- 1
- Maombi yanayoendelea
- 2
Ramani
Roadmap
Phase 1: Pilot Iringa — usajili, ukaguzi, kadi ya kidijitali, na uthibitishaji wa umma. Kisha upanuzi wa kitaifa kwa mikoa yote kwa hatua.
Uhakiki
Thibitisha uanachama
Ingiza namba ya uanachama (mf. GEA-000001) au skana QR kwenye kadi.
Maswali
Maswali yanayoulizwa mara kwa mara
Jiunge na mtandao wa kitaifa
Wasilisha maombi yako leo — kuwa sehemu ya Chama Cha Wahitimu Wajasiriamali Tanzania.